BAKIZA
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita (wa pili kushoto) akizindua Jarida maalumu la Jahazi la Kongamano la tatu Katika Kongamano la Saba la Kiswahili la Kimataifa lililofanyika Tarehe 10-11/12/2023 Katika ukumbi wa Sheik Idriss Abdul Wakil Zanzibar.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita (wa kwanza kulia) akikagua bidhaa za Wajasiria mali katika banda la Maonesho katika ufunguzi wa Kongamano la Saba la Kiswahili la Kimataifa .
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka nchi mbalimbali walioshiriki katika Kongamano la Saba la Kiswahili la Kimataifa lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar.
Makamu wa pili wa Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali pamoja na Watendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Polisi Ziwani - Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na viongozi wengine wa Serikali ya Mapindunzi ya Zanzibar kukagua Maonesho ya vitabu katika Kongamano la Idhaa la Kisahili Duniani lililofanyika Zanzibar
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mh. Fatma Hamad Rajab akizungumza na washiriki wa Konagamano la 6 la Kiswahili lililofanyika tarehe 17-18/12/2022 katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo Wete Pemba
Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar Dkt. Saade Said Mbarouk akizungumza na washiriki wa Konagamano la 6 la Kiswahili lililofanyika tartehe 17-18/12/2022 katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo Wete Pemba

KARIBU BARAZA LA KISWAHILI LA ZANZIBAR

Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) ni taasisi iliyoanzishwa kwa sheria Na. 4 ya mwaka 2004 ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. BAKIZA lipo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Chombo hiki kimeundwa kwa madhumuni ya kusimamia masuala yote yanayohusu lugha ya Kiswahili, matumizi, maendeleo, mafanikio na changamoto zake Zanzibar.

 
Dkt. Shein na Maendeleo ya Kiswahili Zanzibar

Tsh. 6,000/=

Utamaduni wa Mzanzibari

Tsh. 5,000/=

Kamusi la Lahaja la Kitumbatu

Tsh. 10,000/=

Kamusi la Lahaja la Kipemba

Tsh. 10,000/=