BAKIZA

KUTOA USHAURI

Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) linatoa ushauri kwa Wanafunzi na Wataalamu wa Kiswahili, Washairi na Wapenzi wa lugha ya Kiswahili juu ya matumizi sahihi, fasaha na sanifu ya Kiswahili kupitia vipindi vya redio, televisheni na makala katika vijarida, magazeti na machapisho.
Pia, BAKIZA linatoa ushauri kwa Waandishi wa vitabu ili kuweza kuandika vitabu na machapisho mbalimbali vinavyohusiana na lugha ya Kiswahili.