BAKIZA

KUELIMISHA

Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) linatoa taaluma kwa jamii juu ya matumizi sahihi fasaha na sanufu ya Kiswahili katika taasisi za umma nna binafsi kupitia vipindi vya redio televisheni na makala katika vijarida, magazeti na machapisho. Pia BAKIZA linaandaa na kuendesha mafunzo, mijadala, midahalo, semina na makongamano kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu, wanafuzni, wanahabari, watumiaji na wadau wengine wa Kiswahili kwa lengo la kupata fursa ya kujadili na kubadilishana mawazo kitaaluma.