BAKIZA

MAJUKUMU YA BAKIZA

Bakiza lina kazi nyingi ambazo zinajiegemeza katika maeneo muhimu yafuatayo:-

  •   UELIMISHAJI

Kutoa taaluma kwa jamii juu ya matumizi sahihi, fasaha na sanifu ya Kiswahili katika taasisi za umma na binafsi kupitia vipindi vya redio, televisheni na makala katika majarida na magazeti. Kuandaa na kuendesha mafunzo, mijadala, midahalo, makongamano na semina kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu, wanafunzi, wanahabari na wadau wengine wa Kiswahili na kupata fursa ya kujadili na kubadilishana mawazo kitaaluma.

  •   UHARIRI

Kuhariri miswada ya vitabu vya Kiswahili na nyaraka nyengine kutoka taasisi na watu binafsi na kutoa ithibati juu ya usahihi wa lugha iliyotumika.

  •   UCHAPISHAJI

Kutoa machapisho ya Baraza kama vile majarida, makamusi, makala, vitabu, vipeperushi na miongozo mengingine kwa lengo la kuendeleza Kiswahili.