BAKIZA

BWANA MOHAMED SULEIMAN MOHAMED

Alizaliwa tare 5 Oktoba 1943, Kijijini Koani katika sehemu ya kati ya Kisiwa cha Unguja. Alianza uandishi wa hadithi fupifupi mnamo miaka ya 1967/68. Hadithi yake kubwa ya mwanzo, KIU ilishinda katika uandishi wa riwaya Afrika Mashariki ikachapishwa na East Africa Publishing House na kutunukiwa zawadi ya mwanzo mwaka 1970 na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Nyerere. Katika mwaka 1973 riwaya yake nyengine, NYOTA YA REHEMA ilishinda mashindano ya Afrika Mashariki na kutunukiwa Kenyatta Prize for Literature, Kenya na kuchapishwa na Oxford University Press Nairobi.

Hadithi zake fupi zimekusanywa katika kitabu chake kiitwacho KICHEKO CHA USHINDI na kuchapishwa na Shungwaya Publishers, Nairobi Kenya. Kadhalika, hadithi hizo zilitumika katika vipindi vya hadithi fupi katika idhaa ya BBC na Shirika la Utangazaji la Ujerumani, Deustsche Walle.


Tarehe 21 Juni mwaka 1940 ndiyo siku aliyokuja duniani. Uzawa wao wamezaliwa watoto tisa nao ni 1. Saad Shafi, 2. Rukia Shafi, 3. Arafa Shafi (Marehemu), 4. Adam Shafi, 5. Mohammed Shafi, 6. Salma Shafi (Marehemu), 7. Ali Shafi, 8. Zawadi Shafi, na 9. Fatma Shafi.


MOHAMED SULEIMAN MOHAMED aliajiriwa kuwa Mhariri wa Kiswahili wa East African Publishing House, Dar es Salaam mwaka 1977 na baadaye akawa Meneja wa tawi la East African Publishing House Tanzania hadi shirika hilo lilipovunjika wakati wa kufungwa mipaka ya Tanzania na Kenya.


Mnamo mwaka 1982, Mohamed Suleiman Mohamed alianzisha kampuni yake ya Ychapishaji, Educatioal Books Publishers Ltd, Dar es Salaam na kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo hadi sasa. Miongoni mwa vitabu vilivyochapishwa na Educational Books Publishers Ltd ni vitabu vya kiada, ziada na rejea vya masomo yote vibavyoendana na mihutasari ya Tanzania vya madarasa yite kuanzia Darasa la Kwanza hadi Kitado cha Sita.